Majaliwa asema Serikali inandaa karantini za bure, atoa maelekezo kibao

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ipo katika mpango wa kuandaa karantini za bure kwa ajili ya wagonjwa wa Corona hapa nchini.

Majaliwa amaesema hayo leo Machi 2 wakati nchini kukiwa kumeripotiwa visa 13 mpaka sasa.

Licha ya awali Serikali kusema kuwa watakaokwenda Karantini watajigharimia amesema maeneo hayo yatakayotengwa washukiwa wa Corona watakuwa wakikaa bila malipo na yatakusa na huduma zote muhimu.

Majaliwa ambaye leo alikutana na kamati ya kukabiliana na Corona ameitaka Wizara ya afya kuhakikisha inapeleka maeneo yenye uhitaji na kamati hiyo kufuatilia na kuhakikisha watakiwa wanaenda karantini.

Amewasisitiza Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima lengo likiwa ni kuhakikisha Watanzania wanakuwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *