Mahakama ya Zanzibar imesitisha kusikiliza kesi kwa siku 30 sababu ya Corona

Mahakama ya Zanzibar yasitisha shughuli zote za mahakama kwa siku 30 ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

Agizo hilo limetolewa leo na Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar Muhamed Ali Muhamed kutosikiliza kesi hadi Aprili 24 mwaka huu.

“Kesi ambazo ziko katika hatua ya kusikilizwa mahakama itawaruhusu mawakili au wenye kesi kuwasilisha kwa maandishi,” amesema

Aliongeza kuwa “Mahakama zitashughulikia kesi za dharura na kwa washtakiwa wenye kesi nzito na maombi ya dhamana, muombaji na wakili wake au kwa ombi la dhamana wadhamini ndio watakaoruhusiwa kuingia Mahakamani,” amesema.

Amesema kwa makosa yenye dhamana, majaji na mahakimu wanatakiwa kutoa dhamana yenye masharti nafuu ili kupunguza mrindikano katika Magereza kwa kipindi hiki.

Aidha, ameeleza  hakutakuwa na kesi ya madai wala jinai na kuhusu kesi ndogo zitakazotokea ikiwemo kesi za wizi watazungumza na jeshi la Polisi kuhakikisha kesi hizo wanazimaliza

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *