Rais Magufuli ampandisha cheo kuwa Mkurugenzi Mkuu Takukuru baada ya kuokoa Bilioni 8.8

Rais John Magufuli amesema ni jambo la kushangaza fedha zinaibiwa Sh bilioni 8.8 na viongozi wa serikali wapo kimya bila kuchukua hatua.

Kadhalika, Rais Magufuli amempandisha cheo Kaimu Mkurugenzi wa Taasisis ya Kuzui na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Bregadia Jenerali John Mbungo kuwa Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo baada ya kuokoa Sh bilioni 8.8.

“Hii inatugusa sisis viongozi tuliopewa majukumu ya kusimaimia kazi, Takukuru imeeleza wizi uliokuwa unafanyika ameokoa fedha zilizokuwa zimeibiwa Sh. bilioni 8.8.  Swali la kujiuliza hao viongozi waliokuwepo katika eneo hilo wanalipwa mshahara ina maana hakuna mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkurugenzi, viongozi wa chama hamkuona huo wizi,” alisema Rais

Aliongezea kuwa “Hatuwezi kila inapotokea matatizo tunasubiri PCCB haiwezekani sisi viongozi tunafanya nini kwa nini tunakuwa na haya madaraka? Kwa nini mpaka chombo kinachoshughulika na rushwa kiwarudishie wananchi pesa zao ambazo wamelima wao kwa nguvu zao lakini wamezulumiwa,” alisema Magufuli

Brigedia Mbungo

“Ninawapongeza PCCB kwa kazi nzuri mliyoifanya tena nafikiri hutakiwi kuwa kaimu kuanzia leo uwe moja kwa moja kabisa kama umeweza kurudisha Sh. bilioni 8.8 utarudisha mabilioni mengine ambayo yanazulumiwa kwa Watanzania umetimiza wajibu wako pamoja na chombo chako pamoja na kwamba wapo wabaya wachache katika chombo chako hasa huyu wa Kinondoni na watu wake wane najua hiyo issue naifahamu kama yupo hapa hapa na ajue ndio ubaya wangu nachapa hapa hapa,” alisema Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *