Lema: Kauli ya Rais kusema hawataahirisha Uchaguzi ni jambo nzuri ila ajue bila Tume haitawezekana

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema kauli ya Rais John Magufuli kwamba virusi vya Corona haitabadilisha ratiba ya Uchaguzi Mkuu ni kauli safi.

“Jambo muhimu anapaswa kuzingatia ni kwamba uchaguzi Mkuu bila mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi ni hatua ambayo haitawezekana,” aliandika Lema.

Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kuwa Tume iliyopo sasa ni Tume ya uteuzi Mkuu.

Lema aliandika ujumbe huu “Kauli UA Mh Rais John Magufuli, kwamba Corona Virusi haitabadilisha ratiba ya Uchaguzi Mkuu ni kauli safi, jambk muhimu anapaswa kuzingatia ni kwamba Uchaguzi Mkuu bila mabadiliko ya Tume ya Uchaguzi ni hatua ambayo haitawezekana kwani tume iliyopo sasa ni Tume ya uteuzi Mkuu,” alisema Lema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *