Kifo cha kwanza cha Corona charipotiwa nchini Kenya, Afrika Mashariki

Kenya imetangaza kifo cha kwanza cha mgonwa aliyekuwa akiugua virusi vya corona na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza Afrika Mashariki mtu mwenye virusi hivyo kufariki.

Duru kutoka nchini humo zinaeleza kuwa muathirika huyo raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 66 nyakati za mchana katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Agha Khan ambako alikua amelazwa.

Raia huyo ambaye alikua akiugua ugonjwa wa kisukari alikuwa amewasili nchini Kenya Marchi 13, 2020 akitokea Afrika Kusini kupitia Swaziland.

Taarifa ya Serikali ya Kenya ilisema kwamba imepokea kwa huzuni habari za kifo cha Mkenya huyo ambaye alikuwa amekutwa na virusi hivyo baada ya kupimwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *