Dondoo za leo: Mbowe ajitenga na familia akisubiri majibu ya Corona, Wenye mafua kutoruhusiwa kupanda vivuko na Mwendesha bodaboda auawa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News tunatumai uko salama.

Karibu kwenye dawati letu la Dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazobamba nchini asubuhi ya leo Machi 26, 2020.

Habari hizo ni Mbowe ajitenga na familia akisubiri majibu ya vipimo vya Corona, Wenyr mafua kutiruhusiwa kupanda vivuko kulikoni? soma habari hii kwa kina na Mwendesha bodaboda auliwa na kuporwa pikipiki

MBOWE AJITENGA NA FAMILIA AKISUBIRI MAJIBU YA VIPIMO VYA CORONA

Dar es salaam. Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ameamua kujiweka karantini na familia yake baada ya mtoto wake kukutwa na virusi vya corona.

Juzi Katika taarifa yake kwa umma, Mbowe alieleza kuwa  mtoto wake aitwaye Dudley amethibitika kupatikana na virusi vya corona baada ya kupata homa za vipindi, kuumwa kichwa mfululizo na kukohoa kwa siku tano.

Akizungumza jana machi 25. 2020  na Clouds FM katika kipindi cha Jahazi, Mbowe amesema baada ya taarifa hizo ameamua kujitenga peke yake nyumbani Dodoma ambapo anaendelea na shughuli zake huku akisubiri majibu ya vipimo alivyofanya ili kuthibitisha kama amepata virusi hivyo au hakupata.

Soma ziadi>>>

WENYE MAFUA KUTORUHUSIWA KUPANDA KIVUKO
Serikali ya Kenya imesema kuwa itakuwa inawapima wananchi wote wanaotumia vivuko vinavyounganisha Mji wa Mombasa na Kaunti ya Kwale, na wale wote watakaoonesha dalili za mafua hawatoruhusiwa kutumia usafiri huo.

Gavana wa Mombasa, Hassan Joho akitangaza utaratibu huo mpya amesema kuwa watu wote wanaotumia vivuko ni lazima wavalie barakoa, au wafunike midomo na pua zao kwa kutumia kitambaa.

Soma zaidi>>>

MWENDESHA BODABODA AUAWA, PIKIPIKI YAPORWA

Image result for pikipikiMKAZI wa Mtaa wa Stoo katika Kata ya Igunga Mjini wilayani Igunga mkoani Tabora, Maiko Abel (20), ambaye ni dereva wa pikipiki ya biashara (bodaboda), ameuawa kikatili na watu wasiojulikana kisha pikipiki yake kuporwa.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Igunga Mjini, Robert Mwagala alisema mauaji hayo yalifanyika Machi 23, mwaka huu baada ya kijana huyo kukodiwa na mtu mmoja saa tano usiku ampeleke kitongoji cha Makomero.

Alisema kijana huyo alikuwa na pikipiki yenye namba ya usajili MC 757 CAM aina ya pikipiki TVS Star, lakini hata hivyo, hakurudi nyumbani hadi juzi Machi 24 saa nne asubuhi ambako mwili wake ulipookotwa na wachungaji wa ng’ombe ukiwa kwenye palio la ng’ombe nje kidogo na Mji wa Igunga.

Soma zaidi>>>

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *