CAG ailipua jeshi la polisi kufanya malipo ya Sh milioni 193 kwa watumishi waliofariki

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, amesema katika ukaguzi wao wamebaini malipo ya jeshi la polisi kiasi cha sh Milioni 193.13 kwa watumishi 11 ambao wamefariki,kufukuzwa na kustaafu.

Kichere ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa ya ripoti ya CAG ya mwaka 2018/19 kwa Rais John Magufuli.

Alisema katika ukaguzi wao wamebaini fedha hizo kutolewa kinyume cha matakwa ya kanuni ya fedha ya mwaka 2001.

Aidha, amesema kuna taasisi tano za serikali zimefanya manunuzi ya Sh bilioni 5.2 bila kuwepo kwa nyaraka za mikataba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *