Album Ya Harmonize Yapotea Na Kurejeshwa Mtandaoni Ghafla

Album ya AfroEast ya msanii Harmonize imerejeshwa tena kwenye mitandao mbalimbali ya kusikiliza muziki ikiwemo Youtube mara baada ya kutokuwepo kwenye mitandao hiyo jana kutokana na sababu ambazo ameshindwa kuziweka wazi

Katika ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram Harmnize ameomba msamaha kwa mashabiki zake na kuwataka kuendela kusikiliza album hiyo yenye nyimbo 18

“Habari ndugu zangu pole kwa usumbufu uliojitokeza jana kutokana na album yangu ya Afroeast kutokuwepo kwenye mitandao ya kijamii yote..ninapozungumza na wewe album imesharudi kwenye mitandao yote kama Applemusic, Spotify, Tidal, Audiomack na Boomplay na ifikapo saa moja jioni basi itakuwa tayari Youtube” ameandika Harmonize

Ikumbukwe kuwa album hii ya kwanza ya Harmonize ilitambulishwa rasmi Marchi 13 kwenye ukumbi wa mlimani city

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *