Yanga watoa pole kwa Simba, mashabiki waja juu mwenendo hauridhishi

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Yanga wametoa pole kwa Watani zao kufutia kifo cha aliyekuwa msemaji wao.

Asha Muhaji ambaye alikuwa akiisemea klabu ya Simba na mwandishi Mkongwe wa habari za michezo amefariki leo Machi 25, 2020 katika hospitali ya Hindu Mandali jijini Dar ss Salaam.

Salama hizo za rambirambi za Yanga kwa Simba na waandishi wa habari zilitumaa kupitia ukurasa wa klabu hiyo lakini mapekezi yamekuwa tofauti.

Baada ya posti hiyo mashabiki wa yanga walianza kuwaandama na kuwatukana viongozi wa klabu hiyo huku jambo kuu likiwa ni mvutano ulipo baina ya klabu hiyo na muwekezaji ambaye huwajaza mapesa GSM.

Baadhi ya mashabiki wanasema katika klabu hiyo kuna mamluki wanatumwa na klabu ya Simba ili kuivuruga klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani jiji Dar es Salaam.

View this post on Instagram

Salam za Rambirambi

A post shared by Young Africans Sports Club (@yangasc) on

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *