Wenye viwanda Tanzania wajitolea malighafi za kutengeneza pombe kupambana na Corona

Wamiliki wa viwanda mbalimbali hapa nchini wamebadilisha matumizi ya malighafi zao za kutengeneza bidhaa nyingine ili kutengeneza vitakasa mikono (Sanitaizer).

Uamzi huo umechukuliwa ikiliwa ni sehemu ya Mapambano ya kitaifa ya kuubali ugonjwa wa virusi vya Corona ambavyo vinaisumbua dunia na mpaka sasa watu 12 wameathirika nchini.

Kupitia ukurasa wake wa twitter Waziri wa viwanda na biashara wa Tanzania leo Machi 25, amewashukuru wamiliki wa viwanda waliojitolea kuunga mkono vita hivyo.

Kufuatia hatua hiyo ya viwanda huenda bei ya sanitaizer mtaani ikapungua au ikapatikana bure katika baadhi ya maeneo.

View this post on Instagram

Leo nimefanya kikao kilichokutanisha wadau wa Viwanda vinavyotengeneza malighafi zinazotumika kutengeneza Vitakasa Mikono (Hand Sanitizer) kuona namna gani watasaidiana na Serikali katika juhudi za kupambana na virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Corona. – Consumer Choice imetoa lita 10,000 za ethanol na itabadili matumizi ya Ethanol ambayo ilipaswa kutengeneza vilevi ambapo asilimia 75% za Ethanol zitatengeneza Sanitizer. – Mount Meru Millers imetoa lita 10,000 za Sanitizer. – Kilombero Sugar imetoa lita 30,000 za alcohol. Nawashukuru sana wadau wote waliojitokeza leo na tunaendelea kuwakaribisha wengine ili tuunganishe nguvu kwa pamoja kupambana na adui aliye mbele yetu ambaye ni Coronavirus, na kwa kushirikiana kwa pamoja naamini tutashinda na kurudi kwenye lengo kuu la kuijenga Tanzania yenye uchumi wa viwanda.

A post shared by Innocent L. Bashungwa (@innocentbash) on

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *