Siku mbili kuanzia kesho zitaamua umeya wa Meya wa Iringa

Unaweza kusema siku mbili zinazoanza kesho ndizo zitaamua umeya wa Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kibe ambaye chama chake cha siasa ni Chadema.
Baraza la madiwani Iringa mjini litakutana kesho Machi 26, 2020 huku kukitarajiwa maamuzi ya kumvua umeya, Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe.
Barua iliyotolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa hiyo, Hamid Njovu leo Machi 25, 2020  kwenda kwa Kimbe imemtaka kufika bila kukosa ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Kimbe alisema anakabiliwa na tuhuma za mashtaka manne ambayo ni matumizi mabaya ya madaraka, matumizi mabaya ya rasilimali za halmashauri, mwenendo mbaya au ukosefu wa adabu na kushiriki vitendo vya rushwa.
Kupitia akaunti yake ya Twitter Kimbe ameeleza kushangazwa na wito huo wakati kesi ya kutete umeya wake ilikuaa ianza kunguruma kesho kutwa.
https://twitter.com/MayorIringa/status/1242785641659797507?s=19

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *