Rais atangaza uamzi mchungu kukabiliana na Corona, biashara inayoruhusiwa ni ya Chakula tu

Rais wa Uganda Yoweli Museveni amepiga marufuku usafiri wa umma katika nchi hiyo ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona nchini humo.

Hatua hiyo ya Museveni inafuatia kuripotiwa kwa visa 14 vya virusi vya Corona nchini humo ambapo mpaka sasa hakuna aliyepona wala kupoteza maisha.

Katika marufuku hiyo ya siku 14 Mseveni amesema magari binafsi tu ndiyo yataruhusiwa kubebe abiria nao hawapaswi kuzidi watatu akiwemo Dereva.

Amesema katika kipindi hicho cha siku 14 marufuku kufanyika kwa biashara nyingine isipokuwa za vyakula pekee na magari ya kubeba mizigo yataruhusiwa kubeba vyakula.

Amesisitiza raia wake kukaa ndani na kuongeza kuwa magari yote ya Serikali yatakuwa tayari kuwabeba wagonjwa wote isipokuwa magari ya polisi tu.

Government suspends public transport for 14 days

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *