Dondoo za leo: Namna mkono wa Halima Mdee ulivyovunjika, Polepole ahoji kupingwa kwao, kesi yatua Mahakama ya Afrika

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na namna mkono wa Mdee ulivyovunjika, Polepole ahoji na mwisho ni juu ya kesi ya uchaguzi yatainga Mahakama ya Afrika. Karibu;

HALIMA MDEE KUVUNJWA MKONO

X-ray ya mkono wa mbunge wa Kawe (Chadema),Halima Mdee, inayoonyesha jinsi alivyovunjika mkono baada ya kutembezewa kichapo juzi  walivyokwenda kumpokea Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoka gerezani.

Mdee pamoja na Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya wamelazwa katika hospitali ya Agakhan baada ya kutembezewa kichapo na askari magereza wa gereza la Segerea.

Soma zaidi>>>

POLEPOLE AHAOJI

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema haki haitafutwi kwa hisia bila kwa utaratibu.

“Unanihukumu bima kuelewa je nini kilitokea? Tusiendeshwe kwa hisia, haki haitafutwi kwa hisia bali kwa utaratibu,” aliandika Polepole.

“Nini kilitokea mpaka watu wakapigwa ndio swali la msingi. Je watu walipigwa holela? Plus maisha yangu yapo tu, yalikuwepo, yapo na yatakuwepo kama apangavyo Mola,”

Soma zaidi>>>

KESI YAFIKA MAHAKAMA YA AFRIKA

Mwanaharakati wa Katiba, Bob Wangwe akishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamefungua kesi katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR) kupinga wakurugenzi wa halmashauri kusimamia uchaguzi.

Wangwe na LHRC wamefungua kesi hiyo ikiwa imepita miezi mitano tangu Mahakama ya Rufani nchini kutengua hukumu ya Mahakama Kuu iliyokuwa imezuia wakurugenzi hao wa manispaa, majiji na wilaya kusimamia uchaguzi kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangalie jambo hili analohoji mdau juu ya umri sahihi wa kuacha kusema shikamoo kama salamu.

Mdau anasema salamu ya shikamoo kwa jamii yetu ya Tanzania ni ishara mojawapo ya utii na heshima kwa aliyekuzidi umri. Anayesalimiwa huitikia ‘Marahaba’ na kuendeleza kwa maneno ya kujuliana hali

Kuna hoja kuwa watu wazima hufikia wakati hawaitumii tena salamu hii bali hutumia za kujuliana hali kama “Habari za saa hizi” na kadhalika

Anahoji: Je, ni upi umri sahihi wa kuacha kuwasalimia waliotuzidi kwa salamu hii?

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *