Dondoo za leo: Mbatia akana kutumwa na Magufuli Mbeya, Ataka Bashiru apimwe mkojo na Fatma Karume ahoji ukabila sadaka za Gwajima.

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Mbatia kukana kutumwa na Magufuli Mbeya, Lema ataka Bashiru apimwe mkojo kwa kauli aliyoitoa na mwisho ni juu ya Fatama Karume kuhoji juu ya sadaka za Gwajima.

Karibu;

MBATIA AKANA KUTUMWA NA MAGUFULI MBEYA

Mbeya. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema mazungumzo yake na Rais wa Tanzania, John Magufuli ya Machi 3, 2020 Ikulu jijini Dar es Salaam hayakulenga kukiangusha Chadema katika majimbo ya Rungwe, Busokelo na Kyela katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu.

“Nimekuja Mbeya kwenye ziara ya kukiimarisha chama cha NCCR si kwamba nimetumwa na Rais John Magufuli kuja kukiua Chadema. Hiyo ni hofu yao, majungu na ufike wakati kujenga hoja za fikra,” amesema Mbatia jana Jumamosi Machi 7, 2020 katika mkutano na waandishi wa habari mjini Mbeya.

Soma zaidi>>>

WATAKA BASHIRU APIMWE MKOJO

Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema alipoona kauli ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ally Bashiru alimpigia simu Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu kumuuliza kama anavuta gundi.

Lema amesema baada ya kumuuliza Sugu alimkatalia bali akasisitiza kuwa Bashiru anapaswa kupimwa mkojo au akili kwa kauli yake.

Kiongozi huyo aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kwani  ni kauli hatari inayoweza kutolewa na kichaa tu.

Soma zaidi>>>

FATMA KARUME AHOJI UKABILA SADAKA ZA GWAJIMA

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume, amehoji swali kwa mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, wakati akikusanya zile sadaka za waumini huwa anauliza kabila.

“Swali kwa Gwajima wakati wakukusanya zile sadaka za waumini, anauliza kabila za waumini au pesa hazina kabila?,” aliandika Fatma.

Fatma aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake was Twitter kuwa kuna awapishe mbali kuna wasukuma hawataki upumbavu huo.

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangalie  utamaduni huu wa kiafrika wa Mwanamke kumtongoza Mwanaume

Katika utamaduni wetu kama Waafrika/Watanzania, Mwanaume ndio huwa wa kwanza siku zote kueleza hisia zake kwa binti kama anamuhitaji kimapenzi

Hivi sasa imekuwa tofauti kidogo, kuna baadhi ya wasichana wanaanza kueleza hisia zao kwa Mvulana/Mwanaume kama anampenda au anahisia naye kimapenzi

Kwa hapa nchini kwetu inaonekana kama vile Msichana anayemtaka kimapenzi Mwanaume ni muhuni/mapepe/malaya, majina yote hayo anapewa. Tabia hii bado watu wanaona kama si tabia ya kawaida

Je, wewe unaona ni sawa kwa msichana kumtongoza mwanaume au bado tubaki na mila/utamaduni wetu wa mwanaume kumtongoza mwanamke?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *