Dondoo za Leo: Dk. Bashiru amcharua Membe, Lema asema polisi haina taarifa za kuitwa kwake na Mrema aitaka serikali kutoa taarifa ya mchina aliyekutwa na Corona

Habari ya muda huu wasomaji wetu wa Opera News matumaini yetu huu mzima wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazotikisa vichwa vya habari.

Habari hizo ni Dk Bashiru amcharua Membe je unajua ni kwa nini? Soma habari hii kwa kina, Lema asema kaenda polisi kujisalimisha aelezwa hakuna wito wake je unajua nini kitakachotokea? na Mrema aitaka wizara ya afya kueleza kuhusiana na mchina aliyekutwa na virusi vya Corona nchini.

Karibu msomaji wetu ujisomee  habari hizo;

BASHIRU AMCHARUA MEMBE

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, amesema aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje, Bernard Membe, hajafukuzwa uanachama kwa sababu alitaka kugombea urais.

Dk. Bashiru aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha Azam, alieleza kufukuzwa uanachama ni uamuzi wa Kamati Kuu iliyokuwa inatekeleza azimio la Halmashauri.

“Nazungumza kwa tahadhari kubwa mimi matarijio yangu Membe atachukua tahadhari. Kwanza nimesikia kwenye vyombo vya habari habari haijakanushwa eti kosa la maadili ni kutaka kugombea urais,” alisema Bashiru.

Soma zaidi>>>

LEMA ADAI POLISI HAWANA WITO WAKE

Mbunge wa Arusha mjini (Chadema) Godbless Lema, amesema amekwenda ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Arusha hawana taarifa za kuitwa kwake.

“Nimefika ofisi ya RCO Arusha nikiwa na viongozi wa chama, mkoa, wilaya, kanda. Ofisi ya RCO haina taarifa na wito huu,” aliandika Lema.

Soma zaidi>>>

MREMA ATAKA SERIKALI ITOE TAARIFA JUU YA MCHINA ALIYEKUTWA NA CORONA.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ,Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema, amesema ujumbe uliotolewa kuhusiana na  mchina mwenye dalili za ugonjwa wa Corona Tanzania inaogopesha.

Amesema ni vizuri Wizara ya afya ijitokeze iseme wazi na kama huyo mchina kaachwa tu mtaani au yupo chini ya uangalizi.

Mrema alisema uchunguzi maalum angalau kwa siku 14 kama wanavyofanya nchi nyingine dhidi ya mgonjwa huyo.

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo zetu, tujifunze kuhusu kiasi cha maji anachopaswa mtu anywe kwa siku kulingana na uzito

Kama tunavyojua kuwa maji ni uhai, maji yakinywewa kwa nidhamu na kuzingatia uzito mtu alionao tunaweza kukwepa zaidi ya asilimia sitini (60%) ya maradhi mbalimbali.

Muda gani sahihi wa kunywa maji

Mara tu unapoamka asubuhi, nusu saa au dk 45 kabla ya muda wa chakula cha mchana au cha jioni. Muda uliobaki kunywa kiasi kwa kipindi fulani cha muda hakikisha unakunywa maji ukiwa umekaa na kunywa kidogo kidogo.

Muda gani usinywe maji

Usinywe maji wakati au mara tu baada ya kula. Ijulikane kuwa maji na chakula ni vitu viwili tofauti ambavyo mwili unahitaji lakini sio kwa mkupuo. Ukifanya hivyo maji yanaharibu baadhi ya virutubisho vilivyopo kwenye chakula.

Usinywe maji mengi kwa wakati mmoja ili kufikia kiwango kinachohitajika kwa siku. Hakikisha inapofka saa 12 jioni uwe umeshafkia kiwango chako cha mwisho, usinywe maji zaidi ya muda huo yatakuharibia usingizi usiku.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *