Dondoo za leo: Urais wamponza Membe, Maaskofu watoa waraka mzito, Trump awatuliza wamerakani juu ya Corona

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba leo ni pamoja na Membe kufunguka kufukuzwa Ccm, Maaskofu watoa waraka mzito na mwisho ni juu ya Trump kuwatuliza wamarekani juu ya Corona. Karibu;

URAIS WAMPONZA MEMBE

Aliyekuwa kada wa CCM, Bernard Membe amesema amevuliwa uanachama kutokana na nia yake ya kutaka kupambana na mwenyekiti wao, John Magufuli kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Membe na makatibu wakuu wawili wastaafu– Abdulrahman Kinana na Yusufu Makamba– walifikishwa mbele ya kamati ndogo ya udhibiti na nidhamu kujibu mashtaka ya kinidhamu.

Waliingia matatani baada ya sauti zao pamoja na za wanachama wengine watatu, kusambaa katika mitandao ya kijamii zikizungumzia kuporomoka kwa chama hicho na uenyekiti wa John Magufuli.

Soma zaidi>>>

MAASKOFU WATOA WARAKA MZITO

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa waraka wa Kwaresima 2020 ambao mbali na masuala ya uinjilishaji, umezungumzia utawala wa kisiasa, wakisema unatakiwa ufanyike ndani ya mipaka ya sheria ya kimaadili.

Waraka huo wenye kichwa cha habari “Ujumbe wa Kwaresima 2020: Ufalme Wako Ufike”, umetolewa na maaskofu wote 33 wa majimbo ya kanisa hilo nchini Tanzania, wakiongozwa na Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, rais wa TEC.

Soma zaidi>>>

TRUMP AWATULIZA WAMEREKANI JUU YA CORONA

Rais wa nchini Marekani, Donald Trump amewataka wamarekani kutulia na kuondoa wasiwasi baada ya kutangazwa mtu wa kwanza kuwa amefariki kwa virusi vya corona.

Trump amesema amefariki mmoja kwa ugonjwa huo na kuwataka wananchi wake wasiwe na hofu kwa kuwa kuna hatua wanazozichukua kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo zetu tuangazie ukweli kuhusu kung’atwa na mbu

Related image

Huwa inatokea baadhi ya watu wanang’atwa na MBU kuliko wengine, mnaweza kaa sehemu moja na mwenzio ukalalamika unang’atwa na mbu lakini yeye akawa hasikii chochote.

Tafiti zinaonyesha kwamba MBU huvutiwa kunyonya damu ya aina fulani ya watu kama; Mama mjamzito, mtu wenye damu group O, mlevi,  mtu aliyetoka kufanya mazoezi, watu wanene.  #Dr.NormanJonasTweets

Ni hayo tu kwa leo mdau wetu, usisahau kuacha maoni. Asante na siku njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *