Dondoo za Leo : Fatma Karume Amtupia lawama JPM, Polisi yakana kiongozi wa CHADEMA kuuliwa na Kigogo Mradi wa SGR mbaroni

Image result for fatuma karume kabudiHabari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la Dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Fatma Karume Amtupia lawama JPM, Polisi yakana kiongozi wa CHADEMA kuuliwa na Kigogo Mradi wa SGR mbaroni

Fatma Karume Amtupia Dongo JPM

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), Fatma Karume, amesema anahitaji kujua ni kwa nini wakati wakusifu Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Profesa Palamagamba Kabudi anamsifu Rais John Magufuli na serikakali yake.

“Wakati wa lawama za uvunjifu wa haki za binadamu, Kabufi anasema #Tanzania?

Fatma ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa uvunjifu wa haki za binadamu ni dhidi ya Magufuli na serikali yake akiwemo Kabudi na si Tanzania.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Polisi Yakana Kiongozi CHADEMA kuuliwaImage result for Sweetbert Njewike

Jeshi la Polisi mkoani Singida limesema dereva wa bodaboda, Alex Jonas (40) aliyeuawa na watu wasiofahamika alikuwa siyo kiongozi wa Chadema.

Jonas ambaye ni mkazi wa Majengo mjini Manyoni mkoani  Singida mwili wake ulikutwa umepigwa na kitu chenye ncha kali Februari 25, 2020.

Kamanda wa Polisi, Sweetbert Njewike amesema dereva huyo ameuawa Februari 25 mwaka huu nyakati za usiku.

Amesema kijana huyo ambaye kituo chake cha kazi kilikuwa Mwembeni mjini Manyoni bado haijafahamika siku ya tukio, aliondoka muda gani.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Kigogo Mradi wa SGR matatani. Meneja wa mradi wa ujenzi wa Reli ya kisasa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Meneja Uwezeshaji wa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga reli ya kisasa (SGR), Yetkin Gen  Mehmen kulipa faini ya Sh100 milioni au  kwenda jela miaka mitatu  huku ikitaifisha dola za Marekani 84, 850 alizoshindwa kuzitolea maelezo baada ya kukutwa nazo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA)

Mehmen ambaye ni raia wa Uturuki amehukumiwa na mahakama hiyo baada ya kukiri  kosa la kushindwa kutoa tamko ama maelezo ya fedha alizokutwa nazo dola za Marekani 84,850 katika Uwanja wa Ndege wa JNIA

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Ukimaliza kusoma Dondoo za leo tuangalie mambo manne ambayo yanaweza kukusaidia kutokuachwa na mpenzi wako unapokuwa naye kwenye mahusiano

1 Hakikisha unakuwa msafi kwa kila kitu hasa unapokuwa naye.

2. Hakikisha unampa uhuru wa kutosha mnapokuwa mnafanya mapenzi, namaanisha awe na maamzi juu ya mwili wake usimlazimishe kama hayuko tayari, umuandae kabla ya kuanza kumtomasa.  La muhimu sana uhakikishe anafika kileleni kila unapofanya naye mapenzi kwa sababu hii ndiyo hatua ya mwanamke kutambua uanaume wako.

3. Umjengee mazingira ya kukuomba kufanya mapenzi anapojisikia si kufuata ratiba zako tu.

4.Usimfanye akasirike anapokuwa na wewe hata kama kakosea mweleze kwa busara na ikiwezekana uwe unahakikisha anafurahia kila jambo lako; namaanisha fanya mambo anayoyafurahia mara nyingi

Siku Njema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *