Zitto ampa za uso Musiba amuambia hana habari naye

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema ameona video ya mwanaharakati Crprian Musiba akiwa anaongea kwa kutetemeka na mwenye hofu kubwa.

Zitto amesema Musiba amedai maisha yake yapo hatarini kwa sababu yake.

Kiongozi huyo aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake Twitter huku akisema anamuonea huruma sana Musiba kwa hofu aliyokuwa nayo.

“Mimi nimeleta mzungu kutoka Ujerumani ili kumuua. Nimemuonea huruma sana kwa hofu kubwa aliyokuwa nayo.  Namuambi Musiba kuwa Yeye sio adui yangu na wala sina muda kuhangaika naye. Mimi nahangaika na kuhami demokrasia ya nchi yetu ambayo ipo hatarini baada ya kubakwa na Serikali ya CCM ya Awamu ya Tano. Yeye Musiba anatumwa tu na watu wenye maslahi wasiotaka kuona nchi inakomaa kidemokrasia.”

“Waliomtuma aongee Jana ndio wanataka kumwua halafu Mimi na wengine waliotajwa tupewe kesi ya mauaji. Bwana Musiba awe makini na maisha yake kwani waliokuwa wanamtuma wamemchoka na sasa wanataka kumtoa kafara ( kumwua) kisha wazushe kesi ya mauaji kwangu na wakosoaji wengine.”

“Mpango wa Dola kubambika kesi isiyo na dhamana dhidi yangu ni wa muda mrefu. Niliwaumbua kwenye kesi ya money laundering. Sasa wanataka kumwua Musiba na yeye kama zuzu ananituhumu. Sipotezi muda wangu hata chembe kumfikiria Musiba. Nahangaika na mwenye Mbwa. Sihangaiki na Mbwa”Aliongeza Zitto

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *