Serikali kuwabana madalali nchini ili kukusanya mapato

Serikali imepiga marufuku madalali ambao hawana leseni kufanya shughuli hizo kuanzia kesho lakini leseni inapatikana Wizara ya Fedha na Mipango kwa Sh150,000.

Marufuku hiyo inawahusu madalali wote wakiwemo ya nyumba na viwanja ambo kwa Dar es Salaam ni wengi hivyo kuanzia kesho huenda wakapotea mmoja mmoja.

Katibu Mkuu wa Wizara ya fedha na mipango Doto James leo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa leseni za udalali na uendeshaji wa minada amesema hakutakuwa na huruma.

James amesedma kuanzia kesho Serikali itaanza kuawashughulikia madalali wote feki na wanadishaji feki (ambao hawana leseni) kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa sharia kwani uwepo wa watu hao umekuwa ukiinyima Serikali mapato.

“Tutakuwa wakali sana Tumepoteza mapato mengi hata Serikali imewahi kuingizwa mkienge kwa kuwapa tenda watu ambao sio rasmi, lakini sasa nisema madalali feki sasa hamtawaona tena mtaani mtakutana nao Kisutu,” amesema James.

Amesema uzuri madalili wanafahamika na wengi wapo mitaani na wanajitangaza na mabango yao wameweka na mawasiliano hususani Dar es Salaam hivyo kwetu itakuwa ni rahisi kuwapata na kuwashughulikia.

“Hatutakuwa na huruma tena tutakuwa wakali mapato mengi yamepotea, madalali watakaokamatwa tutawatangaza katika vyombo vya habari, nitoe wito kwa wananchi wote na Taasisi za Serikali kufanyakazi na madalali na wanadishaji wenye leseni,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *