Majaliwa ajikingia kifua, Wabunge na Madiwani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi na wanachama wa CCM washirikiane na wabunge na madiwani waliopo sasa na wasiwavuruge wawaache watekeleze majukumu yao hadi pale muda wao utakapomalizika.

Itakumbukwa kuwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarijiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ruangwa kwa tiketi ya CCM ameyasema hayo leo (Ijumaa, Februari 21, 2020) wakati akizungumza katika Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma. Waziri Mkuu ni mlezi wa CCM wa mkoa wa Kigoma.

Waziri Mkuu amewataka viongozi na wanachama wa CCM wajiepushe na suala la ukabila na udini katika kuteua mtu wa kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho na badala yake wateue mtu ambaye anauzika ndani na nje ya chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *