Sheikh aomba huruma ya Mungu virusi vya Corona kuingia nchini

Sheikh wa Mkoa wa Dar es salaam Alhad Salum ameomba huruma ya Mungu kuikinga Tanzania na maradhi ya virusi vya Corona ambayo hivi sasa vinaisumbua nchi ya China.

Sheikh Salum amesema hayo wakati alipopewa nafasi ya kuomba katika Kongamano la Kitaalamu la Chama cha Madaktari nchini (MAT), ambapo Rais Magufuli alikuwa mgeni Rasmi.

“Nakuomba kupitia mkutano huu, utuweke mbali, utukinge na utulinde na Corona Virus isiweze kuingia katika nchini hii wala majirani zetu, tuepushe na magonjwa ya hatari,” ameomba Sheikh.

Amesema anaomba hivyo kwa baraka za manabii waliotumwa na Mungu na sio kwa ndimi za binadamu zilizojaa uongo mapungufu na dhambi bali kupitia kwa watukufu waliotangulia.

Kabla ya hapo sheikh alimshukuru Mungu kwa Rehema zake huku akinukuu maneno ya Mungiu yasemaayo endapo mtaninishukuru nitawazidishia.

Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na madaktari hapa nchini akisema hakuna mwenye uwezo wa kuwalipa.

Aidha alipongeza maendeleo yaliyopo katika sekta ya afya hapa nchini huku akimuomba Mungu kuendelea kumuongoza Rais Magufuli ili aendelee kuongoza vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *