Mbunge wa Chadema azuiliwa kufanya mkutano wa hadhara

Mbunge la polisi wilayani Momba limemzuia mbunge wa Chadema jimbo la Tunduma Frank Mwakajoka kufanya mkutano wa hadhara.

Mwakajoka alipanga kufanya mkutano huo katika shule ya msingi Tunduma Tarehe 23 mwezi huu kuanzia saa 7 mchana hadi saa 12 jioni.

Barua ya kuzuia mkutano huo iliyotolewa na Mkuu wa Polisi ya walaya ya Mambo imeeleza kuwa sababu za kuiwa kwa mkutano huo ni taarifa za kiintelijenshia ambazo zinahatarisha usalama.

“Hii inatokana na uwezekano wa kutokea kwa vitendo vya uvunjifu wa amani katika mkutano huu kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia tulizonazo,” amesema.

Aidha jeshi hilo lilishauri mkutano huo uufanye baada ya hali ya usalama na amani kurejea katika mji wa Tunduma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *