Mbunge Lema: Kuwakalisha washtakiwa kwa muda mrefu mahakamani ni uonevu

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema mahakama inapaswa kutambua kuwa washitakiwa wanaofika  mahakama kwa ajili ya kesi zao wanastahili heshima na utu.

“Mtu anafika mahakamani saa mbili asubuhi kisha shauri lake linaitwa saa nane mchana,” aliandika Lema

Kiongozi huyo aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa huo ni uonevu unaoondoa sura ya mahakama katika kujali na kutenda haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *