Mbunge Heche aendelea kumcharua RC Gambo amuita mjinga

Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, amemtolea povu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kufuatia kauli aliyoitoa kuwa watu wakionyesha barabara mbovu washitakiwe kwa kuhujumu uchumi.

Heche amesema kuna mjinga mmoja anakaa kwenye ofisi ya umma analipwa mshahara, anapewa bima, nyumba, gari na mafuta ya watu wanaoteseka huku kwenye barabara mbovu.

Heche aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter kuwa mtu huyu anasema mtu akionyesha ubovu huo wa barabara washtakiwe kwa kuhujumu uchumi.

Aliandika ujumbe huu ” Mjinga mmoja anakaa kwenye ofisi ya umma analipwa mshahara, anapewa bima, nyumba, gari na mafuta ya watu wanaoteseka huku kwenye barabara mbovu.. Then anasema eti watu wakionyesha ubovu  huu wa barabara washtakiwe kwa kuhujumu uchumi wanataka mapambio na kusifiana ,” aliandika

Hivi karibuni Gambo aliagiza jeshi la polisi kumkamata aliyesambaza video ya ubovu wa barabara katika hifadhi ya Ngorongoro.

Alieleza kitendo hicho cha kusambaza picha hiyo katika mitandao ni kuhujumu uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *