Lema azidi kutibua aweka picha ya gari kukwama arusha kijembe hujumu uchumi

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema,  azidi kutibua hali ya hewa aweka picha ya gari iliyokwama.

Lema baada ya kuweka picha hiyo ya gari iliyokwama kutoka na ubovu wa barabara¬† aliandika ujumbe huu ‘Hujumu uchumi’.

Lema aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter.

Hivi karibuni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliagiza jeshi la polisi kumkamata aliyesambaza picha inayoonyesha miundombinu mibovu katika barabara ya hifadhi ya Ngorongoro kukamatwa.

Gambo alidai kuwa aliyefanya kitendo hicho ni kuhujumu uchumi wa nchi na kwamba akamatwe na kushtakiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *