Kuelekea mechi ya Watani wa jadi Mashabiki wa Yanga waanza Zogo wadai ushindi.

Wakati klabu ya Yanga ikiendelea na maandalizi kuwakabili wagosi wa kaya (Coastal Union) katika mchezo unaofuata mashabiki wake wamechachamaa wakisema wanataka ushindi.

Katika ukurasa wa Instagram Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara waliposti ratiba ya mechi zake 6 zijazo hadi Machi 12.

Katika mechi hizo sita moja Yanga itakutana na mtani wake wa Msimbazi ambaye ndiye bingwa mtetezi wa ligi hiyo (Simba) siku ya Machi 8.

Hata hivyo Yanga ambayo imepata matokeo ya sare kwa mechi zake tatu mfululizo mashabiki wake wameanza kuzoza na kudai ushindi tofauti na siku za nyuma ambapo walikuwa wakiwatia moyo.

Mashabiki wanasema wanashindwa kutamba kwa watani zao na matumaini ya kuwafunga katika mchezo ujao ni madogo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *