Dondoo za leo; Bashiru alivyotumika kuijenga Chadema, Afariki polisi wakizima fujo, Waliobambikiziwa kesi kuchomolewa

Habari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba siku ya leo ni pamoja na jinsi Dk Bashiru alivyoijenga Chadema, Mmoja afariki wakati polisi wakizima ghasia na mwiso ni juu ya waliobambikiwa kesi kuanza kuchomolewa.

Karibu;

KATIBU MKUU CCM ALIVYOIJENGA CHADEMA

UIMARA wa Chama cha Demokrasia (Chadema), ulioonekana kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2015, umechangiwa na Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). 

Dk. Bashiru Ally na Dk. Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, ni miongoni mwa walioshiriki kuandika Sera ya ‘Chadema ni Msingi’ ambayo ilianza kutekelezwa taratibu ambapo sasa imeshika kasi.

Soma zaidi>>>

AFARIKI POLISI WAKIZIMA FUJO

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema John Lulyeho (39) amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi wakati polisi wakituliza vurugu kwenye ranchi ya mifugo ya Mabuki iliyopo Wilaya ya Misungwi.

Akizungumza jana Jumatano Februari 19, 2020 Muliro  amesema Lulyeho alifariki wakati polisi wakimpeleka hospitali ya Wilaya kwa matibabu. Amesema tukio hilo lilitokea Februari 16, 2020 saa 10 jioni.

“Siku hiyo polisi walipokea taarifa kwamba shamba hilo limevamiwa na wahalifu waliokuwa wakiwashambulia  wafanyakazi wa shamba hilo waliokuwa katika hali mbaya karibu kupoteza maisha.”

“Walipofika walikuta wafanyakazi wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Polisi walipofika nao walianza kushambuliwa kwa mawe na askari wetu wawili walijeruhiwa,” amesema.

Soma zaidi>>>

WALIOBAMBIKIWA KESI KUCHOMOLEWA

Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani  nchini Tanzania,  George Simbachawene amewataka watendaji wakuu wa Jeshi la Polisi kuwahoji  watuhumiwa waliopo mahabusu ili kujua tuhuma zinazowakabili, kama wanastahili kukaa rumande.

Amesema lengo ni kudhibiti watu kubambikiwa kesi jambo linalofanyika katika vituo mbalimbali vya polisi nchini, kwamba baadhi ya watuhumiwa wanapelekwa gerezani kwa makosa ambayo hawakuyafanya.

Akizungumza jana Jumatano Februari 19, 2020 katika kikao na watendaji  hao kilichofanyika  makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam, Simbachawene amesema hata Rais John Magufuli anajua kuhusu suala hilo.

Soma zaidi>>>

Tukimalizia dondoo hebu tuangazie kidogo nguvu ya utulivu ukikaa peke yako  kufikiri;

Matatizo makubwa uliyonayo kwenye maisha yako, ni matokeo ya kushindwa kukaa peke yako kwenye eneo tulivu na kufikiria bila ya kuwa na usumbufu wa aina yoyote ile

Ukiwa umekaa karibu na mtu na simu yake ikaita, utaangalia na yako pia. Ukipata dakika chache za kuwa mpweke, haraka sana utakimbilia kuangalia simu yako, kuingia mitandaoni, kufuatilia habari na kadhalika

Asilimia kubwa ya watu wanalala na simu zao, tena zikiwa wazi na hivyo kuruhusu usumbufu hata kama wamelala na wengi kitu cha kwanza wanachofanya wanapoamka ni kuangalia simu zao

Jijengee tabia ya kuwa na muda wa utulivu kwenye kila siku yako, muda ambao unakaa wewe peke yako na mawazo yako, na hakuna usumbufu wowote unaokuwa karibu na wewe katika wakati huu

Mwanzoni utakapokaa tu utaanza kufikiria vitu vingi ambavyo ungeweza kuwa unafanya, mambo mazuri yanayoendelea mtandaoni ambayo yanakupita, lakini usiruhusu hayo yakuondoe kwenye utulivu wako

Anza zoezi hili na utaona jinsi ambavyo maisha yako yabadilika, Msongo utapungua, wasiwasi na mashaka ya kupoteza vitu yataondoka kabisa na utajiona unayaendesha maisha badala ya maisha kukuendesha wewe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *