Mwanamke Ukiwa na Sifa Hizi Ni Lazima Utaachwa Tu

MWANAMKE KIGUU NA NJIA
Sifa ya mwanamke ni utulivu, kama wewe mwanamke una tabia za kupenda kwenda kila unaposikia ngoma au sherehe, wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia hii. Basi kuwe na sababu ya wewe kutoka si kila shughuli ikuhusu wewe.

Wapo ambao hukatazwa na waume zao na kulazimisha kwenda ilimradi tu aonekane naye hajapitwa na sherehe huku akiwa amevaa sare. Kama una tabia hiyo jiangalie.

VISINGIZIO KILA MARA
Wanaume huwa hawapendi mwanamke mwenye visingizio vya mara kwa mara. Hapa naongelea suala la faragha, utakuta mume ana hamu na mke lakini kila akimtajia jambo hilo mara amechoka, mara anaumwa.

Ni kweli una haki ya kueleza unavyojisikia lakini sasa ikiwa ni kila siku visingizio, utasalitiwa kama siyo kuachwa kabisa.

KUMGANDA WAKATI WOTE
Mwanaume anapenda kuwa na mwanamke ambaye atajali pia ‘interest’ zake kwa maana ya kumpa muda wa kufanya mambo yake.

Kuna wanawake wengine wanapenda kuwaganda wanaume wao wakati wote, yaani kwa sababu anampenda basi anataka awe naye wakati wote, hata akitaka kutoka kwenda kwa marafiki zake kubadilishana mawazo na yeye anataka kuwa naye. Huyu atakuwa hajitaki!

MASHOGA WENGI
Wanaume si waumini wa wanawake wanaopenda kuwa na mashoga lukuki au vikundi. Huwachukulia wanawake hao kama wambeya wanaopenda makuu.
Utakuta mwanaume anampenda mwanamke f’lani akimchunguza na kuona ni mwanamke anayependa makundi au ana mashosti kibao huamua kumuacha.

KUMSIFIA ALIYEPITA
Wanawake wengi wakiudhiwa na wanaume wao wawapo kwenye malumbano hupendelea kukumbushia penzi la zamani kwa kusema: ‘Nilipotoka sikuwahi kufanyiwa kama hivi unavyonifanyia sasa.’

KUMPANDA MUME KICHWANI
Wapo baadhi ya wanawake ambao mara nyingi wanapenda waonekane ndiyo wenye sauti ya mwisho ndani ya nyumba. Kwamba akisema kitu mume asihoji, akitaka kufanya lake asizuiwe.

Hili ni tatizo na kwa wasiojua ni kwamba wanaume wengi hawapendi wanawake wenye hulka hii.Kujifanya ‘expensive’

Mwanamke anaweza kuwa kaolewa au yuko kwenye uhusiano na mwanaume wa kawaida ambaye hana pesa kivile na hata akizipata, hana makuzi. Katika mazingira hayo mwanamke anatakiwa kuwa makini sana, akijifanya anapenda makuu anaweza kujikuta anamkwaza mwenza wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *