Mmoja ashikiliwa na polisi, kifo chenye utata mkubwa Serengeti

Jeshi la polisi Mkoani Mara linamshikilia mtu mmoja kufuatia kifo chenye utata ambapo inaelezwa kuwa mwili wa aliekufa umekutwa hauna baadhi ya viungo.

Joseph Juma (42) mkazi wa Morotonga wilayani Serengeti amekutwa amekufa huku baadhi ya viungo vyake kama koromeo na utumbo vikiwa havipo.

Mwili wake umeonekana leo Februari 19, 2020 katika eneo la kitongoji cha Romakendo jilani na daraja la Bwitengi ukiwa mtaroni huku moja ya nguo yake ikiwa kwenye mti.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Daniel Shillah amesema kuwa taarifa za awali ni kuwa walipata ajali kwenye bodaboda aliyokuwa amembeba lakini alikosa msaada wa haraka.

“Tunamshikilia mtu mmoja ambaye alikuwa anaendesha bodaboda kwa ajili ya uchunguzi kwa ajili ya kifo hiki cha mashaka ili kujua kwa undani na taarifa zaidi tutatoa,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *