Hii Ndio Sababu ya Mwanaume Kufikiria Kufanya Mapenzi Kila Baada ya Masaa 48

Umewahi kusikia kauli hizi? ” Mume wangu hatosheki kitandani..” “..Sidhani kufanya mapenzi ndio liwe jambo la msingi lakini huyu mwanaume kaa! Basi tu kila siku mpaka kero..”

Bila shaka ni kilio cha wanawake wachache walioamua kusema. Hivi kweli ni mara ngapi au kiasi gani tuseme inatosha? Je wanaume wanafanya makusudi? Je kuna uwezekano wakabadilika?

Katika mapenzi, suala la kumtaka mwenza kimapenzi hutegemea sababu nyingi, chache ni uwezo wa kiafya, utayari wa kihisia, usalama wa kazini na mengineyo. Japokuwa jinsia zote huwa na kiu ya mapenzi lakini wanaume huwa ni zaidi.

Daktari David Reuben anasema kuwa “.. Wanaume wengi huzungukia ktk mzunguko wa saa 48 yaani huhitaji kukutana kimwili kila baada ya saa 48 ili wawe ktk hali njema ya kimwili na kiakili…”

Nae Daktari na mwandishi Dr Herbert Miles anasema “.. Mwanaume mwenye afya njema mbegu hujaa kila baada ya saa 42 hadi 78 na kuzalisha nguvu kali inayohitaji zitolewe..”

Pia mwanasayansi Alan Frome anasema kuwa ‘.. Wanaume wanaonekana kuwa na njaa ya kukutana kimwili kwa sababu ya maumbile ambapo prostate gland ina kifuko kidogo kitunzacho mbegu, na kijaapo, mwanaume huhitaji kuzitoa, presha huzidi zaidi na zikitoka hurudi ktk hali yake ya kawaida..”

UPANDE WA WANAWAKE
Wanawake hutofautiana kabisaa na wanaume hali kadhalika na wao kwa wao. Kwa mujibu wa utafiti wa Johnson Masters 2010, kwa wastani 20-25% ya wanawake huwa na mtazamo hasi au vuguvugu ktk kuhitaji kukutana kimwili.
2% hawajali kabisa kuhusu kukutana kimwili.

25% zaidi huhitaji sana, husaka kukutana kimwili na huanzisha hitaji hili hata kabla ya mwanaume kusema.
50% iliyobaki huwa na uhitaji wa wastani tu.
Ifahamike pia hasa kwa wanaume kuwa, hali ya mwanamke hubadilika sana ktk kuhitaji tendo la ndoa ktk kipindi cha mzunguko wa siku zake.
Lakini mwanamke anapofikia miaka 40+ hitaji la kukutana kimwili hulingana karibu na lile la mwanaume

NINI KIFANYIKE ?
Wanaume ambao hawajaoa wanapaswa wajike sana ktk shughuli za uzalishaji mali zinazochosha mwili au mazoezi na kuepuka mambo yanayochochea hisia za mapenzi hapo wataishinda saa ya 48, Walio ktk ndoa wawe na utaratibu unaokubaliana na hali ya mwanamke na wajenge mazoea ya kufanya romansi sana ili kuendana na mabadiliko ya mwanaume na kuepusha utumwa wa ngono ndani ya ndoa au kukimbilia nje ya ndoa hali inayoleta magonjwa, kutelekeza familia na mengineyo yasiyoleta furaha ya familia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *