Fatma Karume ashangazwa kuona bei ya roho ya mwanamke ni Sh 300,000 kwa mujibu wa Mahakama

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amesema bei ya roho ya mwanamke wa Tanzania ni sh 300,000.

“Mahakama kuu @judiciarytz imeamua kuwa¬† unaweza kumpiga mke wako mpaka kumuua, hukumu yako itakuwa faini ya sh 300,000,” aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter.

Aliongezea kuwa: “Mnaona sasa athari ya kuwa na majaji wanaochaguliwa na Rais badala kwa uwezo wao?,”

Fatma aliandika ujumbe huu ” Being ya roho ya mwanamke #Tanzania ni TZS 300,000. Mahakama kuu @Judiciarytz imeamuwa kuwa unaweza kumpiga mke wako mpaka ukamuua, hukumu yako itakuwa faini ya TZS 300,000. Mnaona sasa athari ya kuwa na majaji wanaochaguliwa na Rais badala kwa uwezo wao?,”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *