Dondoo za Leo Wahamiaji haramu waterekezwa porini ,Askari amuua mpenzi wake kwa risasi na Atozwa faini kwa kuua bila kukusudia

Image result for wahamiaji haramuHabari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Wahamiaji haramu waterekezwa porini ,Askari amuua mpenzi wake kwa risasi na Atozwa faini kwa kuua bila kukusudia

Wahamiaji haramu waterekezwa poriniImage result for wahamiaji haramu

Wahamiani haramu 61 raia wa Ethiopia, wamekamatwa na Polisi kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji mkoani Morogoro, baada ya kutelekezwa porini na watu wasiojulikana.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Mugabo Wekwe aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba wahamiaji hao, walikamatwa usiku wa Februari 17, mwaka huu katika Kitongoji cha Kwampangile Kijiji cha Doma Tarafa ya Mlali wilayani Mvomero.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Askari Amuua mpenzi wake

Image result for risasi

Askari wa JWTZ Wilayani Nachingwea, Lindi Pascal Lipita(28), amefikishwa Mahakamani akituhumiwa kumuua kwa kumpiga risasi Askari mwenzake ambaye ni Mpenzi wake Baserisa Ulaya, chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

Akisomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa huo Maria Butulaine, Pascal anadaiwa kummiminia risasi 19 Mpenzi wake huyo na kumsababishia kifo wakiwa kwenye kambi ya Nang’ondo,Nachingwea.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Atozwa faini ya laki tatu kwa kumuua mkewe bila kukusudiaImage result for pesa

Mahakama Kuu Kanda ya Kigoma imemhukumu kulipa faini ya Sh. 300,000 mkazi wa Kijiji cha Kiyungwe, wilayani Kasulu kwa kosa la kumuua mke wake kwa kipigo

Akisoma maelezo ya kesi hiyo Wakili wa Serikali, Happy Mayunga, alidai mshtakiwa Msafiri Ntarakila (68) alitenda kosa hilo usiku baada ya kurudi nyumbani kwake akiwa amekunywa pombe na kukuta mke wake hayupo nyumbani.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Tukimalizia dondoo hebu tugusie kidogo juu ya dhana ya baadhi ya watu kuogopa kuomba msaada;

Zipo sababu mbalimbali ambazo zinasababisha watu kuogopa kuomba msaada ikiwemo kupoteza hadhi na heshima katika jamii. Wapo baadhi ya watu wana hadhi fulani ambayo anahisi akiomba msaada kwa watu atadharaulika

Pia, wengine huogopa kukataliwa kwasababu siyo kila ombi linakubaliwa, hofu hiyo huwazuia watu kuomba msaada. Wakati mwingine ukiomba msaada inakuwa ni njia ya watu kufahamu matatizo yako na kuwaambia wengine, jambo linaloweza kutengeneza huzuni ndani ya mtu

Hata hivyo, ni mara chache sana matokeo hasi tuliyoyaona hapo juu kutokea mara tunapoomba msaada

Je, unadhani kuna sababu gani zingine zinazowafanya watu waogope kuomba msaada kwa jamii?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *