Wanywaji Wahofia Maisha Baada ya Kubugia Corona Beer

Matokeo ya picha ya coron beer

Mkurupuko wa virusi vya Corona mjini Wuhan nchini Uchina umesababisha hofi kote duniani huku maelfu wakiripotiwa kupoteza maisha kwavyo na zaidi ya 68,000 kuambukizwa.

Huku shirika la afya duniani (WHO) likitangaza wazi kuwa virusi hivyo ni hatari, wengi wameanza kujihadhari na kujikinga kwa kila namna.

Baadhi ya wanywaji pombe haswa wale wa wanopenda kileo aina ya Corona Beer wameingiwa hofu wakidhani kuwa huenda kileo hicho kina uhusiano na virusi vya corona.

Kutokana na utafiti, imebainika kuwa wengi walijitosa mindaoni kuitafuta na kujua zaidi kuhusu kileo cha Corona na iwapo kinaweza kuwa na uhusiano na virusi vya Corona.

Corona Beer ni kileo cha kifahari ambacho hutengenezwa nchini Mexico na kusambazwa kote ulimwenguni haswa katika nchi za ng’ambo.

Tangu kuripotiwa kwa mkurupuko wa virusi vya Corona, imebainika kuwa uuzwaji wa pombe hiyo imepunguka, wanywaji wakisitisha kuibugia na kuifanyia utafiti kamili.

Matokeo ya picha ya corona virus china

Hata hivyo imebainika kuwa pombe hiyo haina uhusiano wowote na virusi vya Corona ambavyo kwa sasa vimefika bara la Afrika, Misri ikitangaza kisa cha kwanza Ijumaa, Feberuari 14.

Kama njia na kujikinga na maradhi hayo, nchi kadhaa zimesitisha safari za Uchina,  Amerika ikiwaondoa zaidi ya wananchi wao 200 pamoja na maafisa wa serikali  nchini humo.

Virusi  vya Corona viliripotiwa kwa mara ya kwanza Wuhan, Uchina, ripoti zikibaini kuwa kuwa ilitokana na wanyama wa majini walioliwa, ripoti ambazo hadi sasa hazijathibitishwa rasmi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *