Virusi Vya Corona: Balozi wa Kenya Nchini Uchina Ahofia Maisha ya Wakenya Wuhan

Matokeo ya picha ya saraa serem

Balozi wa Kenya nchini Uchina ameonyesha hofu  huku akieleza kuwa hali inazidi kuwa mbaya zaidi kufuatia mkurupuko wa virusi vya corona

Sarah Serema aliwaomba Wakenya kuwaombea wenyeji wao wanaoishi katika mji wa Wuhan nchini Uchina

Alieleza kuwa zaidi ya wanafunzi 100 raia wa Kenya wamekwama nchini humo huku serikali ikisisitiza kuwa kamwe haitawaondoa

Balozi wa Kenya Nchini Uchina Sarah Serem ameonyesha hofu kubwa kuhusu hali ya afya ya wanafunzi wa Kenya ambao wamekwama nchini Uchina huku hali ikizidi kuzoroteka zadi kufuatia mkurupuko wa virusi vya Corana mjini Wuhan.

Kulingana na balozi huyo, ziadi ya wanafunzi 100 wamekwama nchini humo huku serikali ya Kenya ikisisitiza kuwa haina mpango wowote wa kuwaondoa.

Akihojiwa katika runinga ya Citizen nchini humo Februari 17, balozi huyo aliwasihi Wakenya wazalendo kuwaombea wanafunzi hao.

 

”Ukiangalia idadi ya vifo na maambukizi yanavyoongezeka kutokana na virusi hivyo, inanisikitisha nikikumbuka kuwa nina zaidi ya wanafunzi 100 katika mji huo,’’ alisema.

Virusi hivyo ambavyo viligunduliwa mjini Wuhan Uchina mwishoni mwa Disemba 2019 hadi sasa imesababisha vifo vya takriban watu 1,665 na kuwaambukiza zadi ya 68,000.

Hayo yakijiri, Watanzania wanaoishi katika mji huo wamelalamika kuhusu hali yao ya afya huku wakiiomba serikali kuchukua hatua ya kuwaondoa nchini humo ili kuyaokoa maisha yao.

Katika video iliyopchikwa mitandaoni, baadhi yao walilalamika kuhusu jinsi hali inavyozidi kuwa mbaya zaidi huku mamia wakiambukizwa na na wengi kufariki kila kuchao.

Kisa cha kwanza cha virusi vya Corona katika bara la Afrika  viliripotiwa nchini Misri Ijumaa, Februari 14 baada ya mtalii mmoja kupatikana nayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *