Njia Muhimu za Kujikinga na Virusi Vya Corona

Matokeo ya picha ya corona virus china

Mkurupuko wa virusi vya Corona vimesababisha hofu si nchini Uchina tu bali duniani kote, hii ni baada ya kubainika kuwa virusi hivyo husambaa kwa kasi mno na madhara yake ni makuu.

Virusi vya Corona viliripotiwa Wuhan, Uchina mwishoni mwa mwezi Disemba na hadi sasa zaidi ya watu 1,665 wamefariki kwavyo na wenine ya 68,000 kuambukizwa.

Shirika la afya duniani tayari limejitokeza na kutangaza kuwa virusi hivyo ni hatari na tishio kubwa kwa dunia nzima.

Ingawa hadi sasa haijapatikana chanjo ya kuzuia maradhi hayo, WHO na CDC zinapendekeza mbinu zifuatazo kama njia za kujikinga kutokana na virusi hivyo.

Matokeo ya picha ya corona virus china

  • Nawa mikono kwa maji na sabuni kila mara ama kutumia njia nyingine ya kuinadhifisha
  • Hakikisha umefunika mdomo na mapua kwa kutumia sasha ama ukumbo kila wakati unapokohoa ma kucheua
  • Usiyaguse macho, mapua, mdomo kwa mikono ambayo haijanawishwa.
  • Usimkaribie yeyote ambaye ameathirika
  • Usitumie sahani, vikombe, malazi pamoja na vitu vingine ambavyo vimetumika na mwathiriwa.
  • Uwe nyumbani unapotoka kazini, shuleni na ujitenge na umati.
  • Usile nyama ambayo haijacheshwa vizuri
  • Mpashe daktari wako punde unapokuwa na joto ya mwili, taabu katika kupumua na umueleze¬†kuhusu safari zako za majuzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *