Kutana na Muuguzi Aliyekosa Ajira Muda Mrefu Akaamua Kuchuuza Machungwa Mitaani

Unemployed nurse turns to selling oranges on streets after looking for job in vain

Mary Ndoo alihitimu mwaka wa 2007 baada ya kumaliza kozi yake ya uuguzi

Amekuwa akisaka ajira tangu wakati huo bila mafaniko

Ndoo aliamua kuingia katika biashara ya kuchuuza machungwa ili kuweza kukidhi mahitaji yake

Ukosefu wa ajira umekuwa donda ndugu si nchini Tanzania tu bali pia katika mataifa kadha wa kadha.

Banati mmoja aliyetambulika kama Mary Ndoo ambaye pia ni muuguzi amechukua hatua na kuanza kuchuuza machungwa mitaani baada ya kutafuta ajira kwa zaidi ya miaka mitatu bila mafanikio.

Raia huyo wa Ghana alieleza kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya maisha kuzidi kumpiga chenga na kufeli katika kujikidhia mahitaji.

Matokeo ya picha ya hawking oranges

Katika chapisho kwenye mtandao wa Facebok, Oppong Kwarteng  alieleza kuwa banati huyo alihitimu mwaka wa 2017 katika chuo cha uuguzi cha  Zuarangu.

Kwa zaidi ya miaka miwili alisaka ajiri katika mahospitali kadhaa bila matumaini kabla kuamua kutembea mitaani kwa uteo kichwa akichuuza machungwa hayo.

Katika chapisho hilo, Opong aliisihi wizara ya afya kuingilia kati na kuwapa ajira wanafunzi hao waliohitimu na wamekosa ajira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *