Dondoo za leo: Mtume Mwamposa aja kivingine, Uzuiaji Maiti hospitali wapigwa Stop, Master Jay aogopa kuoa kisa Stamina,

Image result for MwamposaHabari yako mdau wa Opera News, tunatuamai uko salama.

Karibu kwenye dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini siku ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Mtume mwamposa aja kivingine, Uzuiaji maiti Hospitalini sasa wapigwa stop, Master Jay aogopa kuoa kisa Stamina

MTUME MWAMPOSA AJA KIVINGINE

Image result for MwamposaMtume Bonifance Mwamposa amekuja kivingine na kutangaza leo ni upako wa kula keki badala ya kukanyaga mafuta.

Mtume Mwamposa ambaye anatuhumiwa katika kesi ya vifo 20 vilivyotokea katika ibada aliyokuwa anaiongoza mkoani Kilimanjaro ambapo wakati wa kukanyaga mafuta watu 20 walifariki katika kugombea kukanyaga mafuta na kujikuta wakikanyagana.

Katika tangazo lake lenye kichwa cha habari Inuka Uangaze likieleza kongamano kubwa la kula keki ya upako litakalifanyika leo Februari 16, 2020.

Soma zaidi>>>

UZUIAJI WA MAITI HOSPITALI SASA WAPIGWA STOP

Image result for ummy mwalimuWAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amepiga marufuku hospitali nchini kuzuia maiti kutokana na gharama za matibabu na badala yake zibuni njia za kudai malipo hayo.

Katazo hilo alilitoa hivi karibuni jijini Dar es Salaam, alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Tawi la Mloganzila, kuangalia kero na vikwazo wanavyopata wagonjwa wanaopatiwa matibabu.

Alisema anafahamu lipo tatizo la wananchi kushindwa kumudu gharama za matibabu na ikizingatiwa kuwa hospitali hiyo inatoa huduma kwanza kabla ya kudai malipo.

Soma zaidi>>>

MASTER JAY AOGOPA KUOA KISA STAMINA

Image result for master jay

Dar es Salaam. Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Joachim Kimaro maarufu Master Jay amesema ana jambo la kujifunza baada ya ndoa ya msanii wa Bongofleva, Stamina kuvunjika.

Ametoa kauli hiyo baada ya mtayarishaji huyo kushauriwa na mmoja wa mashabiki zake amuoe mpenzi wake, Sarah Kaisi.

Sarah maarufu  Shah ni  msanii wa Bongofleva aliyewahi kutesa na wimbo wa ‘Sugua Gaga’, amekuwa katika mahusiano na Master Jay kwa muda mrefu.

Soma zaidi>>>

Kumalizia dondoo zetu tuangazie suala la wivu katika mahusiano

Image result for being too jealousyDk. Norman Jonas, Mtaalamu wa masuala ya Afya ya Jamii anaeleza kwamba kuna wivu wa mapenzi wa kawaida na kuna ugonjwa wa wivu wa wapenzi.

Anasema, tatizo la akili la wivu wa mapenzi huitwa OTHELLO SYNDROME ambapo  Mtu anagandwa na fikra kuwa mpenzi wake sio mwaminifu bila sababu na kuwa na tabia zisizo za kawaida za wivu.

Tatizo la akili la Othello limepata jina kutoka kwenye hadithi moja ya Shakespears ambayo ndani yake kuna mhusika anaitwa Othello ambaye alimuua mke wake kwa sababu ya hisia kuwa mke wake hakuwa mwaminifu, hisia ambazo hazikuwa kweli.

Tofauti na wivu wa kawaida, watu wenye tatizo la akili la Othello huwa na vitendo vilivyopitiliza visivyo kawaida vya wivu kama kukagua simu, kumtembelea ghafla kazini au nyumbani ili kufumania, kupiga simu mara kwa mara ili kujua mtu yuko wapi na yupo na nani.

Vitendo vingine ni kuajiri watu wa kufuatilia nyendo za mpenzi wako kukagua vitu kama mikoba nk. ili kupata vithibitisho, wengine hukagua hadi sehemu za siri za wapenzi wao ili kupata ushahidi wa kusalitiwa Tatizo hili la akili hufikia hatua ya unyanyasaji wa kijinsia, kifo au kujiua.

Je wivu wako ni wa kawaida au ni tatizo? Usisahau kutuachia maoni yako mdau wetu, asante na siku njema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *