Zitto amjibu Bashiru amuambia wameenda nje ya nchi kueleza CCM inavyobaka demokrasia

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amemjibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally na kumueleza wamekwenda nje ya nchi kueleza ubakaji wa demokrasia unaofanywa na CCM.

“Ndugu Bashiru tumekwenda Ulaya, Amerika na Afrika. Tumezungumza na serikali za Afrika kusini, Nigeria na Ethiopia kuhusu ubakaji wa demokrasia ambao CCM mnafanya,” aliandika Zitto.

Aliongeza kuwa:”Mlipotaka kutufuta tulizungumza na Namibia (SWAPO) ili wawashauri. Hakuna propaganda tena dhidi yetu #Tumehuru,”

Zitto aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter akijibu taarifa ya Bashiru aliyodai kuwa wengine wapo Ulaya wanatafuta huruma msikubali kutishwa nao.

“Msitishwe nao wanatafuta huruma ya refa na wanasema refa sio huru wala hawajasajili hawana mchezaji wala mashabiki,” alisema Bashiru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *