Dondoo za leo : Upinzani kufutwa Nchini,Dole la kati lamponza mtumishi na Pesa za mafuta zaitia matatani City

Image result for chademaHabari ya asubuhi mdau wa Opera News, tunatumai u bukheri wa afya.

Karibu katika dawati la dondoo tupate kukujuza habari tatu zinazoshika vichwa vya habari nchini asubuhi ya leo.

Zinazobamba ni pamoja na Upinzani kufutwa Nchini,Dole la kati lamponza mtumishi na Pesa za mafuta zaitia matatani City

Upinzani KufutwaImage result for mangula na jpm

Makamu mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula amesema chama hicho tawala nchini Tanzania kitashinda viti vyote vya udiwani, ubunge na urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020 na kuvifuta vyama vya upinzani.

Ametoa kauli hiyo wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza alipokutana na viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani Sengerema.

Amesema mwaka 2020 ni wa uchaguzi, CCM lazima ihakikishe inashinda, kuwataka viongozi kufanikisha jambo hilo kwa kuteua wagombea sahihi ili kuepusha malumbano.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Dole la kati lamponza Mfanyakazi MgodiniImage result for tanzania football federation mwadui fc

Mchezaji wa Mwadui Hashim Yahya Mussa amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kwa kosa la kuwaonyeshea kidole cha kati watazamaji kama ishara ya matusi baada ya filimbi ya kumaliza mchezo ilipopigwa.

Kitendo hicho kilifanyika katika mchezo uliochezwa Februari 8, 2020 katika uwanja wa Namfua mjini Singida.

Hata hivyo sharia kwa mchezaji anayefanya kitendo hicho ni kali na huenda mchezaji huo akafungiwa hata mechi tano au zaidi.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Pesa za Mafuta zaiponza CityImage result for man city player sad

Umoja wa vyama vya soka Ulaya (UEFA) umetangaza kuifungia club ya Man City ya England kwa misimu miwili mfululizo kwa kutenda makosa mawili.

Kwa mujibu wa UEFA ni kuwa Man City imefungiwa (2020/21 & 2021/22) kushiriki michuano ya Ulaya ngazi ya club na faini ya pound milioni 24.9 (Tsh bilioni 74.9) kwa kosa la kuvunja sheria za UEFA za leseni ya vilabu na Financial Fair Play.

SOMA ZAIDI>>>>>>>

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *