Ajibu, Mzamiru na Miraji kuikosa mechi ya Lipuli, Kocha asema wapo Fit

Wakati Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Simba SC wakiingia dimbani leo kuwakabili Wanapaluhengo (Lipuli FC) imeelezwa kuwa itawakosa nyota wake watatu.

Katika mchezo huo utakaopigwa uwanja wa samora Simba itakosa huduma na ufundi wa Miraji Athuman, Mzamiru Yassin na Ibrahim Ajibu.

Kwa mujibu wa Meneja wa Klabu hiyo Patrick Rweyimamu Miraji na Mzamiru wataukosa mchezo huo sababu ya Majeruhi na Ajibu ameomba ruhusa ili kushughulikia mambo yake ya kifamilia.

Hata hivyo timu hiyo jana ilifanya mazoezi ya mwisho na Kocha wa Wekundu hao wa Msimbazi Sven Vandenbroeck amesema timu iko fit na maandalizi yamefanywa kuhakikisha timu hiyo inashinda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *