Zitto: Takukuru wanaangaika kubumba ili wanipe kesi kwenye Tegeta Escrow lengo nisishiriki Uchaguzi Mkuu siogopi

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe, amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wanataka kumkamatisha kwenye sakata la Tegeta Escrow.

Zitto amesema wanabumba tuhuma zingine kwenye Tegeta Escrow kwa lengo la kumuweka ndani kwa muda mrefu ili asishiriki Uchaguzi Mkuu.

“Ninawaambia tena siogopi. Takukuru  waache kufanya kazi kama jumuiya nne ya CCM, Wazazi, wanawake, vijana na Takukuru,” aliandika Zitto

Zitto aliandika ujumbe huo leo katika ukurasa wake wa Twitter  huku akisisitiza kuwa wasidhani anaogopa kurudi Tanzania “Nitarudi mchana kweupe”.

” Nitakuwa mahakamani kusikiliza hukumu ndogo ya kesi yangu ya uchochezi na pia kesi yangu dhidi ya Rais @ MagufuliJP kuvunja katiba ya nchi kwa kumfuta kazi CAG. Zote siku UA jumanne tarehe 18/2/2020,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *