Zitto aibukia deni la taifa asema deni la nje ya nchi ni Dola bilioni 24

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema deni la taifa  la nje ya nchi limefika Dola za kimarekani bilioni 24 hadi januari 2020.

Zitto aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akiekeza kuwa deni la taifa la nje kwa mwaka 2015 lilikuwa Dola za Kimarekani bilioni 15.

Aidha, amesema deni la taifa la ndani hadi januari 16, 2020 lilifika Sh. trilioni 16 na mwaka 2015 lilikuwa Sh trilioni 8.

Zitto amesema mikopo kutoka benki ya biashara imefikia asilimia 37 ya deni la nje kutoka asilimia 29 mwaka 2015.

Kiongozi huyo ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini ameeleza kuwa takwimu za Benji Kuu ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *