Yajue mambo ambayo wanawake wanayapenda usije kujidanganya wanapenda fedha tu


Habari ya muda huu wasomaji wetu ninakukaribisha katika ukurasa wetu wa mahusiano ili uweze kujifunza mambo mbalimbali.

Katika mahusiano kuna mambo mbalimbali ambayo kila mmoja anapaswa kuyajua ili aweze kulinda mahusiano yake.

Sasa leo nitazungumzia suala la baadhi ya wanaume kudhani kuwa mwanamke huwa anapenda pesa zaidi katika mahusiano.

Nataka niwatoe katika fikra hizo usije ukazani kumpa pesa mwanamke ndio kupendwa katika mahusiano. Nataka nikujulishe kuwa mwanamke anaweza kukupenda bila hizo pesa zako.

Usitangulize fedha katika mahusiano ukazani ndio kujenga mahusiano. Unaweza ukawa ni mtoaji wa fedha lakini humjali mwanamke wako kwa vile fedha inakupa jeuri.

Fedha ni chombeza katika mahusiano lakini kikubwa wanawake wanachopenda ni kujaliwa yaani kubembelezwa. Wanawake wengi wanapenda kupembelezwa kumuonyeshea ile love yako ni ya ukweli kutoka ndani ya moyo wako na sio kutumia fedha kuonyesha unampenda.

Hivi utajisikiaje unapewa fedha lakini upendo katika mahusiano hakuna. Utasikia mwanaume anakuuliza kwani unakosa nini kila kitu nakupatia sawa unampatia kila kitu lakini anamisi kubembelezwa.

Asikuambie mtu kubembelezwa kuna raha yake sijui kama mnanielewa vizuri ila mwanamke ukimbembeleza kama inavyotakiwa hata shida zake anazisahau.

Sasa kuna hawa wanaune hawajui kubembeleza wao kazi yao ni kutumia fedha. Hivi fedha inaweze kushawishi kubembeleza ukajihisi upo ulimwenge mwingine? Wanaojua kubembeleza au kumthamini mke wake hapa ananielewa vizuri.

Wanamume nataka kuwaambia kubembelezwa kwa mwanamke kuna raha yake kuliko hata hizo fedha zako hakuna raha kama hiyo katika mahusiano japo wanaume wengi hawajui.

Wengi wao wanaona fedha ndio kila kitu katika mahusiano. Hujawahi kuona mwanamke ana fedha zake lakini anatoka nje ya ndoa yake tena anaanzisha mahusiano na mtu wa kawaida hujawahi kujiuliza ni kwa nini? Je anafuata hela? Wakati mwingine anatafuta kubembelezwa ama kupata amani ya moyo.

Utakuta mwanaume ndani ya nyumba ni mkali utazani simba lakini anakutimizia mahitaji yako tatizo linakuja katika penzi mnapokuwa faragha au na maeneo mengine hajui kubembeleza yeye ni amri mwanzo mwisho.

Kwa mwanamke kama huyo hata umpe fedha kiasi gani hawezi kufurahi mahusiano ya aina hayo. Fedha isikufanye ushindwe kumpa malove love mpenzi wako.

Kwa mfano mimi napenda kubembelezwa kokote nitakapokuwa naye haijalishe nipo faragha au laa.

Unajua mnaweze kubembelezana hata kama mwanaume wako hana hela ndani ya nyumba mkajiona mna hela kwa sababu wote mna amani ya nafsi. Katika mahusiano cha kwanza kinachoangalia ni amani ya moyo na sio fedha.

Masuala ya fedha katika mahusiano hayo ni mbwembwe tu kikubwa ni kuelewana na kumfanyie mwenzako yale ambayo anayataka ili kumfanya awe na amani na kuendelea kuyafurahia mahusiano yenu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *