Virusi vya Corona bado vinaitesa China, Vifo zaidi vyaongezeka

Image result for balozi wa china tanzaniaUbalozi wa China nchini Tanzania umesema mpaka jana Februari 11, watu 1,380 walikuwa wamefariki dunia kutokana na virusi vya Corona.

Taarifa iliyotolewa na ubalozi huo leo Februari 14, 2020 inasema mpaka sasa watu 63,851 ndiyo wameripotiwa kuwa na virusi hivyo katika Jamhuri ya China.

“Katika hao ambao wameripotiwa 6,723 wametibwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, wengine 55,748 bado wanendelea na matibabu huku 10,109 wakiwa wanasubiri vipimo vya majibu,” ilieleza taarifa hiyo.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Afya, nchini Tanzania Dk Faustine Ndugulile amewahakikisha Watanzania kuwa nchi bado iko salama na hakuna mgonjwa yeyote mwenye ugonjwa wa Virusi vya Corona.

“Niseme tu kuwa Tanzania mpaka sasa hivi bado tuko salama na hakuna mgonjwa yeyote ambaye ameripotiwa na amethibitika kuwa na ugonjwa” amesema Dkt Ndugulile.

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikifuatilia taarifa mbalimbali za washukiwa na watu wote ambao tunawahisi kuwa na ugonjwa huo na tumeweza kuwapima na kubaini kuwa hawana ugonjwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *