TCRA imezifungia laini za simu zaidi ya milioni 7, bado wanaendelea kufungia

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema mpaka sasa wamezima laini za simu za mkononi milioni 7.3.

Kwa mujibu wa taarifa ya usajili hadi tarehe 12 Februari 2020, jumla ya Laini zote za simu zilizounganishwa mitandaoni ni 43,777,515.

Idadi ya Laini zilizosajiliwa kwa alama za vidole ni 32,948,073 sawa na asilimia 75.3 ya laini zote.

Aidha, Laini zilizozimwa ni 7,316,445 na tayari watumiaji wa laini 1,790, 646 wamerudisha laini zao kwa kusajili kwa alama za vidole hadi kufikia hiyo tarehe 12/02/2020 na hivyo kufanya idadi ya laini zilizozimwa kubakia 5,525,799

“Idadi ya laini ambazo bado hazijasajiliwa kwa alama za vidole ni 10,829,442 (zenye wamiliki takribani 3.5m hivi) ambazo zilisajiliwa kwa kutumia kitambulisho cha Mpiga kura na Mzanzibari Mkaazi. Uhakiki kwa kushirikiana na NIDA unaendelea na utaratibu wa kuzifunga unatekelezwa,” taarifa huyo ilieleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *