Tanzania Prisons yapewa pointi za bure na magoli matatu

Timu ya Tanzania Prisons imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kwenye mchezo uliotakiwa kufanyika Februari 11, 2020.

Uamzi huo unakuja umetolewa kutokana na Ruvu Shooting ambayo ndiyo timu mwenyeji kushindwa kuleta gari la wagonjwa (Ambulance) uwanjani.

Taarifa iliyotolewa leo na Shirikisho la Soka (TFF) imeeleza kuwa uamuzi huo ni kwa mujibu wa kanuni ya 14 (2l) jambo lililosababisha mchezo kuvunjwa na mwamuzi baada ya kusubiri kwa dakika 30 bila gari hiyo kutokea.

Katika mechi hiyo iliyokuwa inatakiwa kuanza saa 10 kamili jioni gari la wagonjwa liliwasili saa 10;34 na Prisons waligoma kucheza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *