Sabaya amchokoza tena Mbowe

Image result for sabaya vs mboweNi kama Sabaya amaeanza tena Kumchokoza Mbowe hiyo ni kutokana na kauli zake ambazo zinaweza kutafusiriwa kama uchonganishi kwa wanachama wa Chadema.

Mkuu  wa Wilaya ya  Hai, Lengai ole Sabaya, amemtaka Mbunge  wa jimbo hilo Freeman Mbowe, kufanya  maridhiano  ndani  ya chama  chake , ndipo  aombe maridhiano na Rais John Magufuli.

Sabaya  ameyasema  hayo leo Februari 14, 2020 wakati akiwa katika shughuli za CCM Wilayani hapo, Amesema Mbowe  anapokea   fedha za ruzuku   za  Chadema zaidi  ya sh360milioni na kwamba wanachadema  hawajui zinafanyanini.

“Kama Mbowe anataka maridhiano aanze kwanza kwenye chama  chake  ndipo  aombe maridhiano  na watu  wengine “alisema  Sabaya

Ameongeza kuwa Mbowe  aliwahi  kuchukua  sh600milioni za  chama  na kununua  matrekta  yake  binafsi na kufanya  nayo  biashara  na mkaguzi alipokagua  aliandikia  ni deni  la chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *