Mnyama Tembo azua balaa Morogoro, wananchi waeleza tahadhali za kuchukua

Image result for tembo ajeruhi watuWakati tukifunga safari kutoka maeneo tofauti kwenda mbugani kushangaa wanyama huwa tunadhani wanaokaa karibu na mbuga wanafaidi sana kwakuwa wao wanawaona wanyama kwa urahisi bila gaharama yoyote lakini bana hakuna raha isiyo na karaha.

Unaambiwa Mnyama tembo amewajeruhi watu wawili sehemu mbalimbali za miili yao akiwemo mwanafunzi wa shule ya sekondari ya AlphaJames, Edger Jackson(19) mkazi wa manispaa ya Morogoro na huko ni karibu na mbuga ya Mikumi.

Mwingine aliyejeuhiwa ni John Mhuhu ambaye alikanyangwa na Tembo huyo baada ya muda mfupi akitoka nyumbani kwake ndipo alipomuna tembo akitoka mtoni huku akipiga kelele.

Tukio hilo la kujeruhiwa watu hao limetokea Februari 14, 2010 ambapo Tembo huyo anadaiwa kukatiza maeneo mbalimbali majira ya saa 9 usiku.

Majeruhi wote wawili wamelazwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro wakiendelea kupatiwa matibabu zaidi.

Afisa wanyamapori mkoani humo Joseph Chuwa amesema usumbufu huo umekuwa ukitokea kwakuwa kuna watu wamejenga maeneo yenye njia za wanyama hao.

Chuwa amewataka wananchi kuongeza umakini wa hasa nyakati za usiku ambapo kumekuwa na viashiria vingi vya wanyamapori kukatiza.

“Mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini Tawa wanaendelea kufuatilia nyayo za wanyama hao ili kuhakikisha wanawatoa katika maeneo ya makazi ya watu,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *