Mdude asema mikopo inayokopa serikali ni sawa na mkulima anayekopa kwa mwaka na kupanda miti

Mwanaharakati Nyagali Mdude maarufu kwa jina la Mdude Chadema amesema kwa bahati mbaya serikali inakopa pesa ili inunue ndege, kujenga SGR miradi ambayo haina biashara.

“Yaani ni sawa na mkulima anayekopa bank kwa mkataba wa mwaka halafu yeye anatumia mkopo huo kulipa kilimo cha miti atakayovuna baada ya miaka 15,”

Mdude aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter akiendelea kueleza kuwa lazima deni lizidi kuwa kubwa.

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo aliweka taarifa huku akisema deni la taifa  la nje ya nchi limefika Dola za kimarekani bilioni 24 hadi januari 2020.

Zitto aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Twitter huku akiekeza kuwa deni la taifa la nje kwa mwaka 2015 lilikuwa Dola za Kimarekani bilioni 15.

Aidha, amesema deni la taifa la ndani hadi januari 16, 2020 lilifika Sh. trilioni 16 na mwaka 2015 lilikuwa Sh trilioni 8.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *