Fedha za vitambulisho vya Magufuli zapigwa

Wakati ambapo Watumishi wa umma wanaziona fefha za Serikali kama kaa la moto, kuna watu wanajiamini jamani na hawana woga hata chembe, unaambiwa kuna watu wamepiga pesa za Rasi bana bila woga ila sasa cha moto wanaenda kukipata.

Iko hivi, Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Mtwara imebaini ubadhilifu wa Sh 82.7 milioni kutokana na mauzo ya vitambulisho vya wajasiriamali pasipo kuwasilisha fedha za malipo benki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 14, 2020 Kamanda wa Takukuru mkoa wa Mtwara,
Enock Ngailo emesema waliendesha zoezi maalumu la ufuatiliaji wa fedha za vitambulisho hivyo katika wilaya tatu za mkoa wa Mtwara na kubaini ubadhilifu kwa baadhi ya watendaji.

Wilaya ambazo tayari zimefanyiwa uchunguzi ni Mtwara, Masasi na Tandahimba.

Amesema tangu ufuatiliaji huo uanze Novemba 25, 2019 hadi Feb 13,2020 wamefanikiwa kuokoa Sh 34.1 milioni fedha ambazo zilikuwa hazijawasilishwa benki na zilikuwa mikononi mwa baadhi yawatendaji baada ya kufanya kazi.

“Tumebaini ubadhilifu kwa watendaji wasio waaminifu na katika ufuatiliaji tumebaini ubadhilifu wa Sh 82.7 milioni kutoka ma mauzo ya vitambulisho vya wajasiriamali pasipo fedha kuwasilishwa benki, katika ufuatilia tayari zimeokolewa Sh 34.1 milioni fedha ambazo hapo awali hazikuwasilishwa benki na zilikuwa mikononi mwa baadhi ya watendaji,” amesema.

Ngailo amesema vitambulisho 2,430 sawa na Sh 48.6 milioni fedha zake hazijawasilishwa benki.

“Jumla ya vitambulisho vilivyopokelewa katika wilaya tatu tulizofanya uchunguzi ni 43,000, wilaya ya Mtwara vitambulisho (15,300) Masasi (14,700) na Tandahimba (13,000) kwa maana hiyo wilaya nyingine bado ufuatiliaji unaendelea ili kupata jumla ya vitambulisho ambavyo vilivyotolewa,”amesema Ngailo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *